Saturday, November 4, 2017

JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA MATUNDA

Matunda mbayo hayajaiva sana ni mazuri katika uengenezaji wa jam kwa wepesi kuliko yaliyoivaa sana kwasababu ya acid pectin iliyomo ndan ya hayo matunda ni kubwa sana.ili utengeneze jam iwe nzuri acid  aina ya pectin ni muhimu  sana.
Kutegemeana na matunda uliyo yachagua ,mfano tunaweza kutengeneza jam tamu sana kwa matunda mbalimbali kama ndizi,papai,parachichi,embe,zabibu,zaituni na mengineyo kulingangana na unachokipenda.katika nakala hii utajifunza  namna ya kutumia matunda mbalimbali ambayo unaweza kuyapata kwa uraisi sokonoi au kwenye bustani iliyopo nyumbani kwako.
Watu wengi huzani vitu kama jam vinapatikana tu kwa kutengezwa kwa viwanda na kuuzwa kwenye supermarket kubwa kubwa.ukweli ni kwamba ukiwa hapohapo nyumbani kwako kwa kutumia vyombo na vifaa vichache  vya kawaida waweza kutengeneza jam yako tamu sana.
Hii ndo mifano ya jam ambayo naitengeneza kawa ajili ya kunipatia kipato na pia natumia badala ya siagi kwenye mkate na vitafunwa vingine
1.PAPAI
Tunda la papai ni tamu eh…..
Ni rahisi kupatikana na halina gharama kubwa ,wapenzi ni vizuri ukajaribu kutengeneza mwenyewe jam hii ya papai alafu utaniambia ilivyo poa,,,ni kweli itakua poa tu kama utafuata maelekezo haya jinsi ya kutengeneza kwanzia mwanzo adi mwisho.kipato changu kimekua kwa sababu natenegneza kwa ufasaa na umakini bila  kutumia gharama kubwa.haya twende kazi
MAHITAJI
  1. Chukua papai lako moja au mawili  kg1
  2. Sukari kg 1
  3. Malimao mawil makubwa
  4. Maji safi na salama

NAMNA YA KUANDAAA
  • Osha vizuri kwa maji safi papai lako na uondoe uchafu wote
  • Menya papai kwa kutumia kisu
  • Katakata vidogovidogo na weka kwenye bakuli
  • Saga papai kwa kutumia blenda au kama hauna tumia njia hii:-
  • Mimina matunda yako kwenye sufuria
  • Tia maji kidogo na ufunike
  • Weka sufuria lako jikoni kwenye moto wa wastani kulingana na jiko utakalo tumia kama ni mkaa au gesi au la umeme hakikisha moto ni mdogo wa wastani.
  • Chemsha kwa muda wa dakika 15  huku ukikoroga papai lako na hakikisha imerojeka kama imesagwa kisha uweke juice ya limao uliyo kamua robo kikombe cha nusu lita
  • Anza kwa kuweka sukari kasha tangawizi kwenye papai ulilolipika
  • Chemsha vyote kwa pamoja adi vilainike utaona povu likitoka hii ni kawaida tumia kijiko kuliondoa
  • Epua na usubiri ipoe
  • Weka kwenye vyombo ulivyo andaa ni vizuri ukatumia sterilized jar
  • Utunzaji kwenye friji ni mzuri na unafaa
  • Furaia jam yako na familia au utumie kama fursa ya kukuingizia kipato kama nifanyavyofanya  mimi.





TUTAENDELE NA AINA NYINGINE YA MATUNDA.


KAA KARIBU 

DESHOLILY

No comments:

Post a Comment

Featured Post

JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA MATUNDA Matunda mbayo hayajaiva sana ni mazuri katika uengenezaji wa jam kwa wepesi kuliko yaliyoivaa sana ...